Jinsi ya kutumia Viambatanishi vya PIM
Viambatanishi vya PIM vinaelezea taratibu za utekelezaji wa Program za usambazaji maji vijijini pamoja na awamu za Utekelezaji mbalimbali; ambazo ni; Mipango, Utekelezaji, Uendeshaji na Matengenezo(O&M), na Kujenga uwezo(CD).

Taratibu za kiutawala zinaelezea mchakato wa utekelezaji wa WSDP kiutawala. ”Taratibu za kiutawala zinazohitajika” inamaanisha taasisi zote za utekelezaji zinapaswa kutekeleza michakato yote kama ipasavyo. Ikifanyika kinyume na taratibu,miongozo na makubaliano pamoja na uwajibikaji kwa wadau wa Mpango wa Maendeleo katika sekta ya Maji inaweza kupelekea kusitishwa kwa utoaji wa fedha kwa taasisi za utekelezaji.

Kwa upande mwingine maelezo ndani ya karatasi la kiufundi linampa mtumiaji taarifa za nyongeza kuweza kutekeleza shughuli zilizoelezewa katika ukurasa wa kiutawala. Shughuli zote za kiutawala zinaweza kutekelezwa bila taarifa zilizoko katika kipengele cha kiufundi. Lakini pia kiwango cha utekelezaji kinaweza kuboreshwa kama mtumiaji ataelewa taratibu za kiufundi zilizotajwa katika kipengele cha ufundi. Mitazamo maalum ya kiufundi imetajwa katika kila kipengele cha utawala.

Mambo yote yanayopatikana katika PIM yamewekwa katika mfumo wa Takwimu za computer. Kwahiyo kifaa kinachoweza kuendesha mfumo wa takwimu(database ni muhimu katika matumizi ya taarifa. Ikitokea unapenda kupata Taarifa kupitia MoW HP, unaweza kufanya hivyo kupitia intaneti iliyounganishwa kweye computer (Window, Mac), simu (Androids, iOS) na Smart phones (Androids, iOS, Windows). Mfumo wa takwimu ulioandaliwa kitaalam usiotumia mtandao utapatikana katika DVD wizara ya maji kwa ajili ya taasisi zote za utekelezaji kwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na mtandao wenye uhakika. Mtiririko wa uendeshaji huu umeelezewa kwenye mchoro unaofuata chini.

Operation Flow

Mtiririko wa taratibu za kiutawala zinazopaswa kufuatwa na timu ya halmashauri ya maji na usafi wa mazingira (RWST) kwa utekelezaji wa miradi ya usambazaji maji vijijini na kujenga uwezo.