Jinsi ya kutumia Michakato wa PIM

Michakato ya PIM inaelezea taratibu za utekelezaji wa Mradi wa usambazaji maji vijijini pamoja na awamu ya Mipango, Utekelezaji,Uendeshaji na Matengenezo(O&M), Ufuatiliaji na Ttathmini (M&E) na Kujenga uwezo (CD). Yaliyomo katika Michakato wa PIM yamepangiliwa katika sehemu mbili ambazo ni muundo wa kiutawala na kitaalamu.

Muundo wa kiutawala unaelezea hatua zinazotakiwa kwa utekelezaji katika Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji “Ipasavyo Kiutawala” inamaanisha wakala wote wa utekelezaji wanapaswa kutekeleza michakato yote kwa usahihi. Ikifanyika kinyume na taratibu,miongozo na makubaliano pamoja na uwajibikaji kwa wadau wa Mpango wa Maendeleo katika sekta ya Majiinaweza kupelekea kusitishwa kwa utoaji wa fedha kwa wakala wa utekelezaji.

Kwa upande mwingine muundo wa kiufundi unampa mtumiaji taarifa za nyongeza kuweza kutekeleza shughuli zilizoelezewa katika muundo wa kiutawala. Shughuli zote zinazopaswa kutekelezwa kiutawala zinaweza kutekelezwa bila taarifa zinazopatikana katika kipengele cha ufundi. Lakini pia kiwango cha utekelezaji kinaweza kuboreshwa kama mtumiaji ataelewa mwelekeo wa kiufundi uliotajwa katika kipengele cha ufundi. Mitazamo maalum ya kiufundi imetajwa katika kila kipengele cha utawala.

Mambo yote yanayopatikana katika Michakato wa PIM yatakuwa katika misingi ya Takwimu ya computer. Kwahiyo kifaa kinachoweza kuendesha misingi ya takwimu(database ni muhimu katika matumizi ya taarifa. Ikitokea unapenda kupata Taarifa kupitia MoW HP, unaweza kufanya hivyo kupitia intaneti iliyounganishwa kweye computer (Window, Mac), simu(Androids, iOS) na Smart phones(Androids, iOS,Windows). Msingi wa takwimu unaopatikana katika DVD unatakiwa kupatikana Wizara ya Maji ili Wakala wote wa Utekelezaji ambao maeneo yao hayana intaneti ya uhakika waweze kupata. Mtiririko wa uendeshaji huu umeelezewa kwenye mchoro unaofuata chini.


Operation Flow