Component 2: Rural Water Supply

Overview of PIM Processes for Component 2 (WSDP Phase 2)


 1. Outline of Component 2
 2. The overall objective of Rural Water Supply and Sanitation Programme (RWSSP) is to improve the provision of clean and safe water supply services in rural areas through Local Government Authorities (LGAs). Key implementers of rural water supply and sanitation component are Ministry of Water (MoW), Prime Minister Office-Regional Administration and Local Government (PMO-RALG), Regional Secretariats (RSs) and Local Government Authorities (LGAs). Within the decentralized structures of PMO-RALG, LGAs will facilitate communities to play a leading role in implementation of the water supply projects.

  RWSSP has three sub components intending to improve the different aspects of water supply services. The sub component of “Infrastructure Investment” aims to improve the capacity of the physical infrastructures of water supply facilities in the country by constructing new water supply facilities, rehabilitating existing facilities and expanding the existing facilities. “Capacity Strengthening” is destined to improve the office facilities of RSs and LGAs as well as the soft components such as knowledge, skills, and institutional arrangement for both individual and organizational levels. In addition, “Sustainability of Rural Water Supply” covers other miscellaneous issues such as assistance to Community Owned Water Supply Organizations (COWSOs) in relation to the sustainability of water supply service at the community level.
      
 3. Characteristics of PIM documents
 4. Programme Implementation Manual (PIM) is the operational guideline for Implementing Agencies (IAs) elaborating the institutional arrangement of WSDP, which includes procurement, disbursement of funds, financial management, environmental and social management, monitoring and evaluation, and consists of the main document, volumes and processes. The main document explains the outline of WSDP implementation framework including strategies, focuses/emphasis and components. Processes are the daily reference manuals for Implementing Agencies (IAs) so that staff of IAs shall extract the appropriate information from Processes and carry out actions administratively required in WSDP by following the guidance/procedures explained in Processes.


Mtazamo wa jumla wa Michakato wa PIM kwa Sehemu ya 2 ya Mpango wa Maendeleo wa sekta ya Maji (WSDP 2)
 1. Dodoso Utangulizi wa Sehemu ya 2
 2. Lengo la kuu la programu ya kusambaza maji na usafi wa mazingira vijijini ni kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi na salama katika maeneo ya vijijini kupitia Serikali za Mitaa. Watekelezaji wakuu wa usambazaji wa maji vijijini na kipengele cha usafi wa mazingira ni Wizara ya Maji (MoW), Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa. Katika utaratibu wa mgawanyo wa kazi wa TAMISEMI, Serikali za Mitaa watawajibika kuziongoza jamii kushiriki katika utekelezaji wa Miradi ya maji.

  Program ya kusambaza maji vijijini ina vipengele vidogo vitatu vinavyolenga kuboresha maeneo mbali mbali ya huduma za usambazaji maji.
  1. Kipengele kidogo cha “Uwekezaji kwenye miundo mbinu” kinacholenga kuboresha uwezo wa miundo mbinu ya usambazaji maji chini kwa kujenga miundo mbinu mipya, kukarabati na kupanua miundo mbinu iliyopo.
  2. “Kuimarisha uwezo” Imeelekezwa kuboresha vifaa vya ofisi kwa Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa pia katika maeneo ya uelewa,ujuzi,na mipangilio ya kitaasisi katika ngazi binafsi na Taasisi.
  3. “Usambazaji Endelevu wa Maji Vijijini” Hii inashughulikia mambo mengineyo kama kuzisaidia Jumuia zawatumia maji (COWSO) kuhakikisha ustawi wa huduma za maji katika ngazi ya jamii.

 3. Muonekano/Tabia ya Nyaraka za PIM
 4. PIM ni muongozo wa jinsi ya utendaji kwa wakala wa utekelezaji (IAs), unaofafanua mpangilio wa kitaasisi katika Mpango wa maendeleo wa sekta ya maji (WSDP) inayojumuisha manunuzi,mgawanyo wa fedha, usimamizi wa fedha, usimamizi wa mazingira na jamii, Ufuatiliaji na Tathmini, pia inajumuisha nyaraka kuu, volumes na michakato. Nyaraka kuu zinaelezea muhtasari wa mpango wa utekelezaji ikionyesha mipango,msisitizo na vipengele. Michakato ni rejea za kila siku kwa wakala wa utekelezaji ili wafanyakazi wa wakala wa utekelezaji waweze kupata taarifa sahihi kutoka katika michakato hii ya PIM ili waweze kutekeleza kazi zao kiutawala kama inavyotakiwa katika mpango wa maendeleo katika sekta ya maji kwa kufuata miongozo/taratibu kama zilivyoelezewa katika michakato ya PIM.


Please select your organisation to access the administrative processes to be followed for the implementation of a rural water supply projects and capacity development.

English

CWST                                   RWST
Tafadhali chagua asasi yako ili kupata taratibu za kiutawala zinazotakiwa kufuatwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza maji vijijini na kujenga uwezo.

Kiswahili

CWST                                   RWST